Tuesday 18 August 2015

KITANTWARIKI HIKI








Kaitwa Ouko Oyori, jina kubwa kama kitantwariki,
Kama mvua rasha kanawiri, kwa wako wingi mzaha,
kafanya kozi yao wezi, koni mani kakoni akili wengi,
Hivi leo wewe alumni, lakini katu hukujoini illuminati,
kakataa kukengeushwa nayo campus, kwa madame wake wengi spotless.





Mnamo Septemba mwaka elfu mbili na tisa, Dominiki katoka Kisii,
Guu mosi guu pili, Dominiki kenda Nairobi,
Kabebana nazo begi, zilizojaa kwa wingi mlo,
Si matoke, si maziwa, si mahindi, si ugali, si uji, si ... HEISH!
KAFANANA NA ANAYEHAMA!
Hakutaka katu kukondeana, kwa njaa nyingi yake campus.


Maguo kavalia, green kaunda suit na white reeboks,
Kapendeza kweli kweli, kaitwa 'Gusii land's finest',
Kafanyiwa tamasha ya kufana, ikahudhuriwa na wote watu,
Si mabibi, si mabwana, si machifu, si area Mp,
Kaitwa mwerevu kweli, 'genius wa village yenu'
Kwa shangwe na riboribo, kapandishwa magari Transline



Huyooooooo! Kaja Nairobi, kavukishwa commercial bus station.
HEI! HEI! HEI! Balaa ikaanza .....
Kapotea jiji.
Jiji kubwa la Nairobi!
Hajui aende wapi, hajui atokako,
Kazubaa, kabungaa,
Jengo moja tu alijua...Parliament buildings
Kalijua kwa ziara,"primary school visit to parliament"
Haya mengine yote mageni, hayajui hayatambui.



Bahati katokea, kaonwa na jirani wa  nyumbani,
Huyu kamsaidia kweli, kampeleka hadi 'yunivasiti',
Hayawi hayawi kweli huwa, Dominiki kaingia...
THE UNIVERSITY OF NAIROBI!



Miaka nne ishapita, Dominiki ukaona mengi,
Si mgomo, si msoto, si exile, si supplementary,
Lakini yote kayapiga teke,
Kweli wewe mahiri bingwa...
HOIYEEE!


Written by James Njenga

No comments:

Post a Comment