Wednesday 8 October 2014

KCC TWAENDA





 A.
Gwadiro! Gwadiro! Gwadiro! Mwalimu mkuu ameshikwa!
Kwa ghururi ya maziwa. Maziwa ya KCC.
Mohammed Ali akasema, “ Ni katika parwanja ya ghururi ya maziwa
ambapo mwalimu mkuu wa Soweto primary ametuhumiwa kwa kuwaibia watoto maziwa….”
Lakini sie twajua. Hii ni njama.
Njama ya wivu. Njama ya shule ya Mwambiro
Njama dhidi ya ufanisi wetu kwa mtihani mkuu
Hawatuwezi ngo! Tutawaonyesha cha mtema kuni!
 Watajua hapa kwetu. Mwambiro ni kwao.
Lazima wote twende K...C….C

 B.
Mtaenda pekee yenu. Hatuwajui hatuwang’amui.
Mwalimu mkuu huyo wenu, sisi hatumtambui.
Awapenda hatupendi
Kiyapata maziwa. Sie katupa neti.
 Kiwapa chakula, sie katupa jiwe.
Kiwapa hongera, sie katupa mijeledi
Hiyo ghururi ailipie. Na mazimwi yake nyie.
Hatuendi, sie. Hatueeendi! Abadan






A.
Lakini si sisi wote wamoja? Tumezaliwa wote pamoja?
Tukakomaa wote pamoja? Mwalimu mkuu wetu mmoja?
 Twasomea wote pamoja? Atunasihi wote pamoja.
Maziwa atupa pamoja?

B.
Hatumjui huyo ajinabi. Ni mwalimu mkuu wenu tu!
 Si mwalimu wetu. Yeye ni mwalimu wa kambo.
Mwalimu wetu mkuu ni mzee J. Twampenda twamshangilia.
Lakini huyo wenu, ashughulikie yake macho.
Mpeni hayo maziwa anywe kwanza. Yaache kuwa redi.

A.
Lakini, mbona hivyo…

B.

Tumedhulumiwa. Tumekisiwa.
Tumechukiwa.Tumefelishwa. Tumeadhibiwa
 Kila uchao twalaumiwa. Kutopendwa hakuna raha.
Kuna majonzi mengi eti. Nyie mwafurahi tu.
Lakini hii awamu nyingine, mpende msipende,
 Kweli mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu u mchungu

A.
Hapa hamna nguruwe. Kashfa ni ya ngombe .
Maziwa yake ngombe. Maziwa ya KCC
Nguruwe hazina kitu. Mwalimu mkuu haendi Pork Centre
 Alaumiwa maziwa. Siyo nyama yake nguruwe.

B.
Ni nguruwe.
 A
Ni ng’ombe
 B
Ni nguruwe
 A
Ni ng’ombe

 C
Wanafunzi wanguni. Nisikieni ninenayo.
Hii ghururi ya maziwa nitaiandama.
Hutuma nitazichukua. Tusije kukosana.
Eti mie wenu kuwaletea nuksi. Hivi sasa naondoka.
 Niende huko KCC milk. Tuhuma nizitwange. 
Mambo niyalainishe. Nirudipo niwe msafi.
Bila tuhuma yoyote

B

Twakujua vyema sie. Usije kutuletea balaa.
Na uongo wako huno mwingi. Kusema eti maziwa katuibia sie
Aibu ndiyo huna. Waenda kutuuza.
Tulikuamini na kukuenzi. Hivi sasa wewe mwizi.
Maziwa, uliyapeleka wapi?

C
Siwauzi katu mie. Nawaenzi  wote nyie
. Wakubwa kwa wadogo, nawapenda wote nyie.
 Hii ghururi ni uongo. Maziwa sijaiba.
Ni huyu jirani mwalimu mkuu wa Mwambiro.
Wivu ndio mwingi.
Haambiliki hasemezeki. Aniona mie mwizi.
Hata nitendapo mema. Bado yeye anituhumu.
Lawamu ziso kifaniwe. Amenichusha bin tiki

B.
Na tutakuamini vipi kuwa huendi kutuuza, kutuwacha sie bila mwelekeo?
Kuwafanya hao wanaokutuhumu kutotutia mbaroni?

C
Huu ualimu siendi nao. Nitamwachia naibu wangu
 Awaangalie awatunze. Akae kwa kiti changu.
Akae kwa ofisi yangu. Na aitwe mwalimu mkuu
Hiki kitabu ndicho ishara. Ya mamlaka nilotwikwa.
Mwalimu Serengeti naushike. Wewe ndiwe mwalimu mkuu sasa.
niende niyashughulikie haya mambo peke yangu.
Nikishikwa nishikamane. Nikiachwa na nirudi
Mzima kama kigongo

A na B
Utenda nani? Safari ndefu mwalimu

C
Ndege ndiyo hii. Nitaipanda niende mie.
Kwa sasa kwaherini. Ya kuonana kwaherini.

A
Kitambo  uende tukuambie. Umetufurahisha na weledi,
kujipenda hujipendi. Wapenda yako hii shule.
Uendapo hii blanketi, usipopata pa kulala. Itwike ulalie
Huu nao muhogo, safarini na uule.

B
Aaa mwalimu, moyo wako umejaa upendo
Tumeguzwa nao eti, kukuacha hatukuachi
Uendapo kama kunguni, sisi twakwandama.
Upande na ushuke, sisi tu nawe.
  
A, B na C
KCC natuende. Hii ndege tuipande
Itubebe nasi twende
Ghururi ya maziwa, tuitwike sie wote
Katuathiri sie wote.  KCC tutaenda.
K…C…C.. tunasija!