A. Tumefika, tumefika, tumefiiika.
Kuwanyoosha na kuwanyoa,
Vichwa vyenu naleteni,
Tuwanyoe virembekeni,
Hivi leo tumeamua,
Bila maji kuwanyoa,
B. Kunyolewa hatukatai,
Lakini wembe butu abadani,
Utieni makali jamani,
Usiwe uchungu huno mwingi,
Pia nyinyi vichwa nyooeni,
Muwe gudi roli modeli.
A. Hehehe… kabwela msikie jamani,
Hata marahisi hayajui.
Eti kinyozi hana mnyozi,
Nywele yake i imara tisti,
Haya vichwa mtaleteni,
Tuwanyoe bila maji.
B. Vinyozi shaggi shaggi,
Vyetu vichwa katu touchi,
Hata viwe vingi vidudu,
Uchafu ukolee,
Haviguzwi!
Uchafu ukolee,
Haviguzwi!
A. Hei! Hei! Hei! Kichwa chafu chafaa nani?
Kina wingi wa chawa jamani,
Kina wingi wa kunguni,
Viroboto shereheni,
Wanadhoofisha yako afya,
Kawa mnyonge bin tiki,
Kuja nikunyoe,
Kunyoa kuso maji.
B. Changu kizuri ki chawa,
Chako kibaya ki hujuma!
Changu ki viroboto,
Chako ki maporomoko,
Changu ki kunguni,
Chako chaleta manunguniko,
Wanyoa hujinyoi,
Hata ukinyoa waambukiza vidudu,
Maana chako kibayabaya.
A. Huoni u mbaya,
Hata shuleni kuogopwa,
Wanafunzi kukuavoidi,
Walimu kukugoma,
Huoni u mbaya,
Hata nchi kukukwepa,
Wananchi kukusema.
B. Niwe mbaya au mzuri,
Huniguzi katu!
Kinyozi wewe mahiri,
Jinyoe uninyoe,
Tukae wote smati,
A. Ulosema ndugu kweli,
Yangu nywele kutatiza,
Wananchi kunikwepa,
Eti kwamba natatiza,
Macustomer kunihepa
Eti mimi wao wanakatzika,
Macustomer kunihepa
Eti mimi wao wanakatzika,
A and B.
Naam, nywele baya na defu,
Tuinyoe, inyoleke,
Nchi yetu ifyekeke,
Kusije kubomoke,
Viroboto na chawa,
Vidudu viso haya,
Visafike hapa Saint Pauls.
Naam, nywele baya na defu,
Tuinyoe, inyoleke,
Nchi yetu ifyekeke,
Kusije kubomoke,
Viroboto na chawa,
Vidudu viso haya,
Visafike hapa Saint Pauls.
By James Njenga
No comments:
Post a Comment